

Lugha Nyingine
Vurugu huko El Fasher na Kordofan nchini Sudan yazusha wasiwasi ya Umoja wa Mataifa
Mshambulizi ya hivi karibuni katika eneo la El Fasher la Darfur Kaskazini na vurugu katika eneo la Kordofan nchini Sudan yamezusha wasiwasi ya Umoja wa Mataifa.
Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric amesema mashambulizi yaliyotokea EL Fasher yameathiri vibaya kambi ya wakimbizi ya Abu Shouk na kusababisha vifo vya raia wasiopungua 40 na wengine 19 kujeruhiwa, katika mashambulizi yanayodhaniwa kufanywa na Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF).
Shirika la Uhamiaji la Kimataifa (IOM) likisema njia za kuondoka kutoka katika mji huo zimezuiliwa na kusababisha raia walionaswa kukosa usalama na misaada.
Bw. Dujarric ameongeza kuwa IOM imekaridia kuwa kwenye jimbo la Kordofan Kusini watu zaidi ya elfu tatu wamekimbia kutoka mji wa Kadugli wiki iliyopita, na pia upatikanaji wa misaada ya kibinadamu unakabiliana na vikwazo vingi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma