Wataalamu kuimarisha ushiriki wa vijana katika mambo ya amani na usalama chini ya mfumo wa IGAD

(CRI Online) Agosti 14, 2025

Mkutano wa siku mbili umeanza Jumatano wiki hii mjini Nairobi, kujadili namna ya kuimarisha ushiriki wa vijana katika mapendekezo ya amani na usalama chini ya mfumo wa Shirika la Maendeleo la Serikali za Nchi za Afrika Mashariki (IGAD).

Katibu Mkuu wa shirika hilo Bw. Workneh Gebeyehu alipohutubia mkutano huo, amesema vijana wenye umri wa miaka chini ya 30 katika Afrika Mashariki wanachangia zaidi ya asilimia 60 ya idadi ya jumla ya watu wa eneo hilo. Ameeleza kuwa vijana ni nguvu muhimu ya kulinda amani na usalama katika eneo hilo, lakini wanaendelea kukabiliana na migogoro tata inayodhoofisha uwezo wao.

Amependekeza nchi wanachama wa IGAD ziongeze ushiriki wa vijana katika mambo ya amani na usalama kwa njia ya kutekeleza mageuzi ya sera, na kutoa msaada wa kiserikali kujumuisha jukumu la vijana katika kujenga ustahimilivu wa jamii.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha