Msemaji wa Umoja wa Mataifa: Maeneo 17 ya Sudan yapo katika hatari ya njaa

(CRI Online) Agosti 14, 2025

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric amesema kuwa maeneo 17 ya Sudan, ikiwa ni pamoja na baadhi ya sehemu za Darfur, Milima Nuba, Khartoum na Gezira, yamewekwa katika kundi la maeneo yenye hatari ya njaa.

Akiongea katika mkutano wa kila siku, Bw. Dujarric amesema mwaka mmoja uliopita, njaa ilithibitishwa katika kambi ya wakimbizi ya Zamzam katika jimbo la Darfur Kaskazini mwa Sudan na kuanzia hapo ikaenea katika maeneo ya Darfur na Kordofan. Tangu wakati huo hali hasa El Fasher, mji mkuu wa Darfur Kaskazini, imekuwa mbaya zaidi.

Ameongeza kuwa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limetoa wito wa kutoa misaada ya kibinadamu katika mji wa El Fasher ambao unakabiliwa na njaa na bado haujapatiwa msaada wa kibinadamu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha