Rwanda yajiandaa kufanyika Mashindano ya Dunia ya Barabara ya UCI 2025 mjini Kigali

(CRI Online) Agosti 14, 2025

Rwanda inajiandaa kuweka historia kwa kuwa mwenyeji wa Mashindano ya Dunia ya Barabara ya UCI 2025 kuanzia Septemba 21 hadi 28 katika mji mkuu wa nchi hiyo Kigali, ikiwa ni mara ya kwanza kwa mashindano hayo ya kifahari kufanyika katika Bara la Afrika.

Tangazo hilo lililotolewa Jumatano kwenye akaunti rasmi ya serikali ya mtandao wa kijamii, lilionesha furaha ya taifa hilo kuwakaribisha waendesha baiskeli mashuhuri duniani kushindana katika barabara za mji mkuu.

"Kigali ina furaha kuwa mwenyeji wa waendesha baiskeli bora duniani wanaposhindana katika hafla hii ya kihistoria," ilisema taarifa hiyo.

Ili kuhakikisha ushindani salama na mzuri, mamlaka itafunga barabara kwa muda kwenye njia zilizoteuliwa kwa nyakati maalum wakati wa michuano hiyo ya wiki nzima, iliongeza.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha