China yatangaza aina mpya ya visa kwa wataalamu vijana wa sayansi na teknolojia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 15, 2025

BEIJING, Agosti 14 (Xinhua) – China imetangaza kuanzisha aina mpya ya visa kwa ajili ya vijana wenye vipaji vya sayansi na teknolojia. Waziri Mkuu wa China Bw. Li Qiang amesaini amri ya Baraza la Serikali ya kutangaza uamuzi wa kurekebisha kanuni za nchi kuhusu utaratibu wa kuingia na kutoka kwa wageni.

Kwa mujibu wa uamuzi huo, China itaongeza visa ya K kwenye makundi ya visa za kawaida, zinazopatikana kwa ajili ya vijana wenye ujuzi wa sayansi na teknolojia. Waombaji wa visa hii ni lazima wawe na sifa na matakwa yaliyowekwa na mamlaka husika ya China na kuwasilisha nyaraka zinazounga mkono. Sheria hii mpya itaanza kutekelezwa Oktoba Mosi.

Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Alhamis, mamlaka husika imesema ikilinganishwa na aina 12 za viza zilizopo kwa sasa, visa ya K itatoa urahisi zaidi kwa wanaopewa visa hiyo kwa mujibu wa mara na muda wanaoruhusiwa kuingia, muda wa uhalali na muda wa kuwepo China.

Baada ya kuingia China, wenye viza ya K wanaweza kushiriki katika mawasiliano katika sekta mbalimbali kama vile elimu, utamaduni, na sayansi na teknolojia, na shughuli muhimu za ujasiriamali na biashara.

Kwa kuzingatia umri, historia ya elimu na mahitaji ya uzoefu wa kazi, maombi ya visa ya K hayahitaji mwajiri wa China au shirika kutoa mwaliko, na mchakato wa kutuma maombi pia utaratibiwa kwa umakini. Mkutano huo na waandishi wa habari umesema, maendeleo ya China yanahitaji ushiriki wa vipaji kutoka duniani kote, na maendeleo ya China pia yanatoa fursa kwa watu hao.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha