Wasanii wa sarakasi wa Tanzania warishishana michezo ya sanaa ya China kwa vizazi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 15, 2025

Hamis Adam Nyota (Katikati) akiwaelekeza wanafunzi wake wakati wa mazoezi mjini Dar es Salaam, Tanzania, Agosti 11, 2025.(Xinhua/Emmanuel Herman)

Hamis Adam Nyota (Katikati) akiwaelekeza wanafunzi wake wakati wa mazoezi mjini Dar es Salaam, Tanzania, Agosti 11, 2025. (Xinhua/Emmanuel Herman)

DAR ES SALAAM, Agosti 12 (Xinhua) – Kwenye eneo la Ilala Mchikichini, mjini la Dar es Salaam, Aisha Juma mwenye umri wa miaka tisa, mwanafunzi wa darasa la nne katika Shule ya Msingi ya Ilala Boma, anazungusha mpira kiunoni kwa usahihi. Na kusema huku akitabasamu.

"Ninapenda sarakasi kwa sababu sarakasi inanifanya niwe na afya nzuri na kuona akili yangu."

Simulizi zake ni sehemu tu ya desturi iliyoanza takriban miongo sita iliyopita, wakati vijana 20 watanzania walipotumwa China kujifunza sarakasi, ambayo ilikuwa ni hatua muhimu katika historia ya mawasiliano ya kiutamaduni kati ya China na Tanzania. Mpango huo ulianza kuonekana baada ya kikundi cha sarakasi cha China kufanya maonesho nchini Tanzania na kuwavutia viongozi wa taifa na kuwapa wazo la kuwapeleka vijana wenye vipaji kwenda kupata mafunzo rasmi nchini China.

Mwaka 1965, Hamis Adam Nyota na vijana wengine 19, wakiwa wavulana 14 na wasichana watano, wenye umri wa kati ya miaka 9 na 18, waliwasili mjini Wuhan, Mkoani Hubei China. Licha ya changamoto hizo, walifanya mazoezi kwa bidii kwenye chuo cha Sarakasi mjini Wuhan. Juhudi zao ziliwezesha mkutano wa kihistoria mwaka 1968 na Mwenyekiti Mao Zedong, wakati wa ziara ya Rais wa kwanza wa Tanzania mwalimu Julius Nyerere.

Baada ya kurudi nyumbani mwaka 1969, wanafunzi hao walianzisha Kikundi cha Sarakasi cha Kitaifa, ambacho kilikuwa ni kikundi cha kwanza cha aina hiyo barani Afrika. Chini ya uongozi wa serikali, kilifanya ziara mbalimbali ndani na nje ya Tanzania, na kufanya maonyesho nchini Kenya, Uganda, Zambia, Comoro, na Malawi. Bw. Nyota alikuwa kwenye kikundi hicho hadi mwaka 1977, wakati serikali ilipobadilisha mfumo wa mafunzo ya sarakasi. Alipotumwa mkoani Mtwara, Bw. Nyota aliendelea kufundisha, hata kama wenzake wengi walikuwa wameacha fani hiyo. Yeye pamoja na mwenzake Rajab Zubwa, baadaye walianzisha kikundi cha sarakasi cha kimataifa cha Bantu ili kufufua michezo ya sanaa hiyo.

Mmoja wa wanafunzi wake Saidi Ramadhani Yusuph, sasa ni mkufunzi wa Kituo cha Mafunzo ya Sarakasi cha Happy Centre Acrobatic Talent. Kituo hicho, ambacho sasa kimesajiliwa, kina wanachama zaidi ya 200. Wahitimu ni pamoja na waigizaji wanaojulikana kimataifa kama vile Ramadhani Brothers, walioshiriki kwenye mashindano ya "America's Got Talent," ambacho ni kipindi maarufu cha Televisheni cha Marekani.

Hamis Adam Nyota (rangi nyekundu katikati), kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wake mjini Dar es Salaam, Tanzania, Agosti 11, 2025.(Xinhua/Emmanuel Herman)

Hamis Adam Nyota (rangi nyekundu katikati), kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wake mjini Dar es Salaam, Tanzania, Agosti 11, 2025.(Xinhua/Emmanuel Herman)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha