

Lugha Nyingine
Jumuiya za kikanda za Afrika zaunganisha mipango ili kuhimiza mazungumzo ya amani ya DRC
(CRI Online) Agosti 15, 2025
Rais William Ruto wa Kenya na Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe wametangaza uamuzi wa kuunganisha mipango miwili ili kuhimiza mchakato wa amani kwenye sehemu ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Marais hao waliongoza mkutano maalum wa kilele wa jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na jumuiya ya maendeleo ya kusini ya Afrika (SADC) kwenye mtandao wa intaneti, na kutangaza kuunganishwa kwa mchakato wao wa amani wa Nairobi na Luanda katika mfumo mmoja wa upatanishi unaoongozwa na Afrika, na unaoungwa mkono na Umoja wa Afrika ili kuimarisha usawazishaji.
Ofisi ya rais wa Kenya imesema katika taarifa iliyotolewa Alhamisi kuwa waliidhinisha hati muhimu za uendeshaji na mpango wa kukusanya raslimali ili kuunga mkono mpango huo.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma