Reli ya Mombasa-Nairobi iliyojengwa kwa msaada wa China yatimiza siku 3,000 ya kutoa huduma kwa usalama

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 18, 2025

NAIROBI, Agosti 17 (Xinhua) -- Kampuni ya Africa Star (Afristar) ya uendeshaji wa reli jumapili ilitoa taarifa ikisema hadi kufikia Jumamosi Reli ya Kisasa ya Mombasa-Nairobi (SGR) iliyojengwa kwa msaada wa China nchini Kenya imetimiza siku 3,000 za kutoa huduma kwa usalama. Tangu reli hiyo ianze kutoa huduma Mei 31, 2017, hadi sasa imesafirisha takriban abiria milioni 15.93 na zaidi ya tani milioni 41.96 za mizigo.

Ikiwa na urefu wa kilomita 472 kutoka mji wa Mombasa hadi wa Nairobi, reli ya SGR ya Kenya ni reli mpya ya kwanza kujengwa nchini Kenya tangu ipate uhuru, na pia ni mradi mkuu wa ushirikiano kati ya China na Kenya chini ya pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia moja.

Reli hiyo imesanifiwa, kujengwa na kuendeshwa na Shirika la Ujenzi wa Barabara na Madaraja la China, kwa viwango na teknolojia ya China, pamoja na vifaa na miundo ya usimamizi ya China. Reli hiyo pia imeboresha ufanisi wa usafiri wa Kenya na kuongeza pato la taifa kwa asilimia 1.5.

Wakati wa ujenzi na uendeshaji wake, mradi huo umeleta nafasi 74,000 za ajira na kutoa mafunzo kwa wataalam 2,800 wa Kenya katika teknolojia, na hivyo kuchangia kuongeza ajira za ndani na kuhimiza ujuzi. Kampuni ya AfriStar pia imesema, “Uendeshaji salama wa reli SGR ya Mombasa-Nairobi, si kama tu umeleta njia rahisi na bora ya usafiri kwa watu wa Kenya, bali pia imehimiza maendeleo ya biashara ya ndani na ukuaji wa uchumi.”

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha