

Lugha Nyingine
Mkutano wa 45 wa SADC wafunguliwa nchini Madagascar ukilenga kuimarisha viwanda na kilimo
Mkutano wa 45 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) umefunguliwa mjini Antananarivo, Madagascar, ambapo viongozi wa kikanda wamehimiza uwezo mkubwa wa viwanda na kilimo cha kisasa ili kuendeleza ushirikiano.
Akizungumza kwenye mkutano huo wenye kaulimbiu "Kuendeleza Maendeleo ya Viwanda, Mageuzi ya Kilimo na Mpito wa Nishati kwa SADC Himilivu," Katibu Mtendaji wa SADC Elias Magosi amebainisha kuwa kilimo kinachangia asilimia 33 ya pato la taifa la kanda hiyo na kuingiza mapato ya asilimia 62 kwa wakazi wake, lakini karibu watu milioni 60 bado walikuwa na uhaba wa chakula mwaka 2024. Amesema changamoto hii inadhihirisha uharaka wa mageuzi ya kilimo ili kuhakikisha usalama wa chakula na kuchochea ukuaji, akisisitiza uwezo wa kanda hiyo katika nishati mbadala, hususan nishati ya jua na upepo.
Rais wa Madagascar Andry Rajoelina, ambaye alichukua uenyekiti wa zamu wa SADC kutoka kwa Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa, alisisitiza haja ya kuharakisha ukuaji wa viwanda na kupanua biashara ya ndani ya kanda, akitoa wito kwa nchi wanachama kuonesha umoja na ujasiri katika kutetea maslahi yao ya kibiashara duniani kote.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma