Basi latumbukia mtoni na kusababisha kifo cha mtu mmoja, na wengine 44 hawajulikani walipo katikati mwa Benin

(CRI Online) Agosti 18, 2025

Waziri wa Mambo ya Ndani na Usalama wa Umma Alassane Seidou amesema kuwa basi lililobeba watu 54 lilitumbukia mtoni katikati mwa nchi hiyo mapema Jumapili, na kusababisha mtu mmoja kufariki na wengine 44 hawajulikani walipo.

Basi hilo lililokuwa likisafiri kutoka mji mkuu wa Togo Lome kuelekea mji mkuu wa Niger Niamey, lilitumbukia kwenye Mto Oueme baada ya dereva kugonga kingo ya daraja na kushindwa kulidhibiti gari hilo.

Serikali ya Benin imeanza mpango wa dharura, ikitumia kila njia katika juhudi za uokoaji, na kusema kuwa manusura tisa ambao hali yao sio mbaya sana walilazwa hospitalini. Imetoa salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu na kusema juhudi zinaendelea kuwatafuta waliopotea na kuchunguza chanzo cha tukio hilo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha