

Lugha Nyingine
Rais Trump akutana na Rais Zelensky, viongozi wa Ulaya kuhusu kusuluhisha mgogoro
![]() |
Rais Donald Trump wa Marekani (katikati) akimkaribisha Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine (Kulia) katika Ikulu ya Marekani mjini Washington, D.C. Agosti 18, 2025. (Xinhua/Hu Yousong) |
WASHINGTON, Agosti 18 (Xinhua) -- Rais Donald Trump wa Marekani amewakaribisha Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine na viongozi saba wa Ulaya katika Ikulu ya Marekani, kwa lengo la kusuluhisha mgogoro. Rais Trump alifanya mkutano wa kwanza na Rais Zelensky.
Wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari pamoja na kiongozi wa Ukraine, Rais Trump alisema anaamini Rais Vladimir Putin wa Russia anataka vita iishe, na atashirikiana na Ukraine na pande zote kuhakikisha amani inapatikana.
Rais Trump amesema juhudi zinafanyika kutatua mgogoro na kutakuwa na uhakikisho wa usalama ambao Ukraine inataka. Rais Zelensky alisema anaunga mkono wazo la kumaliza vita kwa njia ya kidiplomasia na yuko tayari kwa mkutano wa pande tatu.
Viongozi hao wa Ulaya (Katibu Mkuu wa NATO Bw. Mark Rutte, Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Ulaya Bibi Ursula Von der Leyen, Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer, Waziri Mkuu wa Italia Bibi Giorgia Meloni, Rais wa Finland Bw. Alexander Stubb, Chansela wa Ujerumani Bw. Friedrich Merz na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron) wamehudhuria mazungumzo ya pande nyingi baada ya mkutano wa pande mbili.
Katika hotuba yake kwa vyombo vya habari pamoja na viongozi wengine, Rais Trump alisema Rais Putin alikubali kuhakikishwa kwa usalama wa Ukraine na kwamba Rais Putin anataka kupata jibu. Rais Zelensky amesisitiza kuwa Ukraine itafurahi kama Rais Trump ataweza kuhudhuria mkutano wa pande tatu unaowezekana pamoja naye na Rais Putin. Rais Zelensky amesema mambo nyeti, ikiwa ni pamoja na suala la ardhi ya Ukraine, yatajadiliwa kwenye mkutano wa pande tatu. Rais Trump amesema mkutano kama huo wa pande tatu unapaswa kufanyika “haraka iwezekanavyo.”
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma