ZEC yatangaza ratiba ya uchaguzi mkuu Zanzibar, kura ya mapema kuanza Oktoba 28

(CRI Online) Agosti 19, 2025

Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imetangaza ratiba kamili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 utakaofanyika Oktoba 29, ambapo kura ya mapema inatarajiwa kupigwa Oktoba 28.

Hii inakuwa ni mara ya pili katika historia ya Zanzibar kwamba kura ya mapema inapigwa siku moja kabla ya upigaji kura ya pamoja, ambapo mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2020.

Akizungumza na wanahabari jana Agosti 18, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji George Joseph Kazi, amesema zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu za uteuzi wa wagombea wa urais, uwakilishi na udiwani litafanyika kuanzia Agosti 28 hadi Septemba 10, 2025.

Aidha amesema tarehe ya uteuzi wa wagombea wa nafasi hizo itakuwa Septemba 11, ambapo kampeni zitazinduliwa siku hiyo hiyo na kuhitimishwa Oktoba 27. Zoezi la kuhesabu kura na kutangaza matokeo ya uchaguzi litafanyika kuanzia Oktoba 29 hadi Novemba 1.

Kwa mujibu wa jaji Kazi, ZEC itahakikisha kunakuwepo na mazingira jumuishi ya kupiga kura kwa watu wenye ulemavu. Kwa mara ya kwanza, tume imeandikisha wapiga kura wenye ulemavu katika orodha ya wapiga kura.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha