

Lugha Nyingine
China yahimiza maendeleo ya utulivu katika mpito wa kisiasa wa Sudan Kusini
Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Sun Lei amesisitiza kwamba kuendeleza kwa utaratibu mabadiliko ya kisiasa nchini Sudan Kusini ni kazi ya dharura.
Akiongea kwenye mazungumzo ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Sudan Kusini, Sun Lei ameongeza kuwa Sudan Kusini ndiyo nchi changa zaidi duniani, na mchakato wake wa kisiasa unatazamiwa kuchukua muda. China inatoa wito kwa pande zote za kisiasa kupunguza tofauti zao kwa njia ya mazungumzo, kuharakisha utekelezaji wa mipango yote ya Mkataba Mpya wa Utatuzi wa Mzozo nchini Sudan Kusini, na kuzingatia suluhu za kisiasa kama njia pekee ya amani. Jumuiya ya kimataifa inapaswa kudumisha ujumuishi na uvumilivu unaohitajika, kuunga mkono juhudi za upatanishi wa kikanda, na kuunga mkono njia za Kiafrika kwa masuala ya Afrika. Pande zote zinapaswa kuheshimu mamlaka, uhuru, na ukamilifu wa ardhi ya Sudan Kusini na kuepusha kutoa shinikizo kwa njia haramu na zisizofaa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma