

Lugha Nyingine
Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati yathibitisha kufanya uchaguzi mkuu Desemba 28
(CRI Online) Agosti 20, 2025
Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) imethibitisha kuwa uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani nchini humo utafanyika tarehe 28 mwezi Desemba.
Katika mkutano wake na maafisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (ANE) mjini Bangui, mji mkuu wa nchi hiyo, waziri wa utawala wa eneo Bruno Yapande amesema kuwa uchaguzi huo lazima ufanyike kama ulivyopangwa, baada ya kuahirishwa mara kadhaa.
Ameongeza kuwa hivi karibuni serikali itaandikisha wapiga kura na kufungua maombi ya kugombea kwenye uchaguzi.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma