

Lugha Nyingine
Watu 13 wauawa kwenye shambulizi la msikiti Nigeria
Kamishna wa usalama na mambo ya ndani wa jimbo la Katsina nchini Nigeria Nasir Muazu alisema watu wenye silaha Jumanne walivamia jamii ya Unguwan Mantau iliyoko eneo la serikali ya mtaa ya Malumfashi, yenye Waislamu wengi, na kuwafyatulia risasi ovyo waumini msikitini wakati wa sala ya alfajiri, ambapo wamesababisha vifo vya watu wasiopungua 13.
Muazu amesema washambuliaji hao walituhumiwa kuwa katika “operesheni ya kulipiza kisasi”, akibainisha kuwa siku mbili zilizopita, wenyeji walifanya shambulizi la kushtukiza dhidi ya majambazi waliokuwa wakisumbua jamii ya Unguwan Mantau na kuwaua “wengi wao”.
Ameongeza kuwa askari wa mashirika ya usalama ya nchi hiyo walisambazwa Jumanne asubuhi wakishirikiana na makundi ya usalama ya jamii hiyo kuzingira eneo hilo na kurejesha hali kuwa ya kawaida.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma