Tanzania kujiandaa na maafa kwa kuchukua hatua za kimkakati

(CRI Online) Agosti 20, 2025

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa ametangaza mipango mikuu mitano inayolenga kuongeza uwezo wa nchi hiyo kukabiliana na majanga ya asili na yanayosababishwa na binadamu, akisisitiza dhamira ya serikali ya kulinda maisha na mali.

Akizungumza katika hafla ya kuadhimisha Siku ya Watoa Misaada ya Kibinadamu Duniani jana mjini Dodoma, Majaliwa alisema hatua hizo zikiwa ni pamoja na kutenga fedha za kujenga upya miundombinu na nyumba zilizoharibiwa, kusambaza vifaa vya msaada wa dharura, kuanzishwa kwa chumba cha hali ya dharura cha kitaifa, na juhudi za kutoa msaada wa kibinadamu kwa kitaalamu, ni sehemu ya juhudi zinazoendelea kufanywa na serikali katika kuimarisha usimamizi wa maafa nchi nzima.

Kwa mujibu wa Majaliwa, tayari serikali imesambaza mbegu, chakula na misaada mingine kwa waathirika wa mafuriko katika mikoa ya Rufiji, Kibiti na Morogoro, pamoja na manusura wa jengo lililoporomoka hivi karibuni katika eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Majaliwa alitoa pongezi kwa wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu, akisifu ujasiri na huruma yao. Pia alihimiza ushirikiano zaidi kati ya wadau ili kuhakikisha ufanisi wa kukabiliana na maafa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha