Maua yapamba mji wa Beijing kabla ya gwaride la siku ya ushindi (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 27, 2025
Maua yapamba mji wa Beijing kabla ya gwaride la siku ya ushindi
Maua kwa ajili ya maadhimisho yanaonekana katika sehemu ya Dongdan mjini Beijing, Agosti 22, 2025. (Xinhua/Ju Huanzong)

BEIJING – Maua yamepambwa katika eneo la katikati la mji wa Beijing, kwenye uwanja wa Tian'anmen na barabara ya Chang'an kabla ya gwaride kubwa la jeshi la China la siku ya ushindi mapema mwezi ujao.

Ofisi ya Misitu na Uhifadhi ya Mji wa Beijing, imesema kuna aina zaidi ya 100 za mimea ya maua yaliyopangwa katika seti 10, na mada inayolengwa ni kukumbuka historia, kuheshimu waliopigania amani, kuthamini amani na kuunda siku zijazo. Baada ya gwaride mapambo hayo yataendelea kuwepo hadi kipindi cha mapumziko ya siku ya taifa ya 2025 mwezi Oktoba.

Gwaride hilo litakalofanyika Septemba 3 mjini Beijing, kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 80 ya ushindi katika Vita vya Watu wa China vya Kupambana na Uvamizi wa Japan na Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha