Aina tatu za ndege za kivita zakamilisha kupaa na kutua kwenye Manowari ya China ya Fujian kwa kusaidiwa na msukumo wa sumaku ya umeme

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 23, 2025
Aina tatu za ndege za kivita zakamilisha kupaa na kutua kwenye Manowari ya China ya Fujian kwa kusaidiwa na msukumo wa sumaku ya umeme
Picha hii ya kumbukumbu ikionyesha ndege za kwenye manowari aina ya J-15T, J-35 na KongJing-600 zikiwa kwenye sitaha ya Manowari ya China ya Fujian. (Picha na Li Tang/Xinhua)

BEIJING – Kikosi cha Majini cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) kimetoa taarifa jana Jumatatu ikisema kuwa ndege za kivita aina ya J-15T, J-35 na KongJing-600 za kutumia kwenye manowari kwa mafanikio zimekamilisha kupaa kwa kusaidiwa na msukumo wa nguvu ya sumaku ya umeme na kutua kwa kasi kwenye Manowari ya Fujian kwa kuvutwa na sumaku.

“Mafanikio hayo yameonyesha kuwa manowari ya kwanza ya kubeba ndege kuundwa na China yenye kifaa cha kurushia ndege imepata uwezo wa kuwezesha ndege kuruka na kutua kwa msukumo na nguvu kinza za sumaku ya umeme, ikimaanisha mafanikio mengine mapya katika maendeleo ya manowari ya China ya kubeba ndege” taarifa hiyo imeeleza.

Ndege za kivita aina ya J-15T, J-35 na KongJing-600 zilionyeshwa wakati wa gwaride kubwa la kijeshi la China lililofanyika Septemba 3 kuadhimisha miaka 80 tangu kupatikana ushindi katika Vita vya Watu wa China vya Kupambana na Uvamizi wa Japan na Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti.

Kikosi hicho cha majini kimesema kuwa, mafunzo hayo yamethibitisha kuendana vizuri kwa mfumo huo wa sumaku ya umeme wa kuwezesha kutua na kupaa kwa ndege ulioundwa na China na aina mbalimbali za ndege.

“Hii inadhihirisha kuwa manowari ya Fujian imepata uwezo kamili wa awali wa kufanya operesheni kwenye sitaha, ikitengeneza njia kwa aina mbalimbali za ndege zinazotumia kwenye manowari kujiunga na muundo wa manowari hiyo” taarifa ya kikosi hicho cha majini imesema.

Katika miaka ya hivi karibuni, vyombo vya anga vinavyotumia kwenye manowari zinazotokana na Kikosi cha Majini cha PLA vimeharakisha maendeleo yake, vikipiga hatua kutoka ndege moja hadi mifumo jumuishi, kutoka vinavyotegemea ufukwe hadi oparesheni za kwenye manowari majini, kutoka urukaji wa kuteleza kwenye sitaha hadi urukaji wa kusukumwa na nguvu ya sumaku ya umeme kwenda juu na kutoka kuwa na uwezo wa kuruka hadi uwezo wa kupigana vita. Kikosi hicho cha majini kinasonga mbele kwa kasi kuelekea lengo la kuwa kikosi cha hadhi ya kimataifa baharini.

Tangu majaribio yake ya kwanza ya baharini mwezi wa Mei 2024, Manowari ya Fujian imekuwa ikifanya mfululizo wa majaribio ya baharini kwa kufuata mpango, ikipiga hatua kwa kufanya uzinduzi wa vifaa na tathmini ya utulivu wa jumla wa kioperesheni.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha