Mikoa ya Kusini mwa China yafanya juhudi zote kukabiliana na kimbunga kikubwa Ragasa (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 23, 2025
Mikoa ya Kusini mwa China yafanya juhudi zote kukabiliana na kimbunga kikubwa Ragasa
Wafanyakazi wakishusha na kuimarisha taa za mitaani mjini Shenzhen, kusini mwa China, Septemba 22, 2025. (Picha na Zhong Zijie/Xinhua)

GUANGZHOU – Ikijiandaa kukabiliana na kimbunga kikali kinachokaribia Ragasa, mikoa ya pwani ya kusini mwa China, hasa Delta ya Mto Zhujiang yenye watu wengi, imesimamisha huduma za treni na feri, kufunga shule na kuimarisha miundombinu ya barabara ili kuhakikisha usalama wa wakaazi wenyeji.

Ragasa, kimbunga cha 18 kilichopewa jina la msimu wa kimbunga cha Pasifiki 2025, kilizidi kuwa kimbunga kikubwa siku ya Jumapili, na kinatabiriwa kuwa huenda kikatua katika maeneo ya pwani ya kati au magharibi ya Mkoa wa Guangdong wa China kesho Jumatano.

Wataalamu wa hali ya hewa wameonya kuwa Kimbunga Ragasa kinasonga kwa kasi huku kikidumisha nguvu zake, ikikifanya kuwa kimbunga chenye nguvu zaidi kuwahi kuikumba China mwaka huu.

Yakiwa yameathiriwa na kimbunga hicho, eneo la kaskazini mwa Bahari ya Kusini ya China na maeneo ya pwani ya kusini mwa China yataathiriwa na upepo mkali na mvua kubwa kuanzia leo Jumanne hadi Ijumaa. Baadhi ya maeneo katika maeneo ya mashariki mwa mikoa ya Jiangsu na Anhui pia yatapata mvua kubwa kutokana na athari za kimbunga hicho, Kituo cha Taifa cha Hali ya Hewa cha China kimesema.

Mamlaka ya Kudhibiti Mafuriko na Misaada ya Ukame ya China jana Jumatatu yalianzisha mwitikio wa dharura wa Ngazi ya IV katika mikoa ya Guangdong, Hainan na Fujian, Wizara ya Usimamizi wa Dharura ya China imeeleza.

Mkoa wa Guangdong siku hiyo ya Jumatatu ulipandisha mwitikio wake wa dharura kwa upepo kwa Ngazi ya II, huku miji mbalimbali ikitangaza mfululizo wa hatua za kusimamisha huduma za umma. Mwitikio wa Ngazi ya II, wa pili wa juu zaidi katika mfumo wa tahadhari wa miji ya ngazi ya nne ya China, ulianzishwa saa 4 asubuhi Jumatatu.

Kutokana na kuathiriwa na kimbunga hicho, mvua kubwa inatarajiwa kunyesha mashariki mwa Guangdong, Delta ya Mto Zhujiang na Guangdong magharibi kuanzia leo Jumanne hadi Alhamisi, huku kukiwa na uwezekano wa mvua kubwa katika baadhi ya maeneo.

Bandari ya barabara kuu ya Zhuhai kwenye Daraja la Hong Kong-Zhuhai-Macao itasitisha huduma za utoaji vibali vya forodha kutoka nje kuanzia saa 9 alasiri leo Jumanne, na daraja kuu litafungwa wakati huo huo, mamlaka za daraja hilo zimetangaza Jumatatu.

Serikali ya Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong imetangaza Jumatatu kwamba masomo katika shule zote yatasimamishwa Jumanne na Jumatano. Kadhalika, mamlaka ya elimu ya Mkoa wa Utawala Maalum wa Macao ilitangaza kusimamishwa kwa masomo kuanzia Jumanne hadi Jumatano kwa shule zote za sekondari, shule za msingi, chekechea na shule maalum.

Mkoa jirani wa Fujian umepandisha tahadhari yake ya kimbunga hadi Kiwango cha III saa 5 asubuhi Jumatatu. Mamlaka ya Kudhibiti Mafuriko na Misaada ya Ukame ya Fujian pia yalipandisha mwitikio wake wa dharura wa kimbunga kutoka Kiwango cha IV hadi Kiwango cha III saa 5 asubuhi siku hiyo hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha