Lugha Nyingine
Viongozi duniani watoa wito wa kudhamiria upya kwa Katiba ya Umoja wa Mataifa
![]() |
| Picha ikionyesha kikao maalum cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuadhimisha miaka 80 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa kwenye makao makuu yake mjini New York, Septemba 22, 2025. (Xinhua/Li Rui) |
UMOJA WA MATAIFA - Viongozi duniani wamehimiza kudhamiria upya kwa ushirikiano wa pande nyingi na kanuni za msingi za kuanzishwa kwa Katiba ya Umoja wa Mataifa kwenye kikao maalum katika Baraza Kuu jana Jumatatu, kuadhimisha miaka 80 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa.
Kaulimbiu ya mkutano wa kihistoria wa mwaka huu -- "Pamoja ni bora zaidi: Miaka 80 na zaidi kwa amani, maendeleo, na haki za binadamu" -- imesisitizwa katika hotuba kadhaa kwenye kikao hicho, kama ilivyo kwa haja ya kuimarisha Katiba ya Umoja wa Mataifa, ambao ulizaliwa kutokana na uharibifu wa vita. Maadhimisho hayo yaliyodumu kwa saa moja yalichanganya tafakuri juu ya historia na miito ya dharura.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kanuni elekezi za Umoja wa Mataifa "zinashambuliwa vibaya kuliko hapo awali," akirejelea migogoro, njaa na machafuko ya tabianchi.
"Ili kukabiliana na changamoto hizi, ni lazima si tu kuutetea Umoja wa Mataifa, lazima tuuimarishe," amesema, akielezea mipango ya mageuzi ikiwemo ile ya Mkataba wa Siku za Baadaye na mpango wa UN80.
"Njia pekee mbele ni kuwa pamoja. Hebu tusimame katika wakati huu kwa udhahiri, ujasiri, na usadikisho. Na hebu tufikie ahadi ya amani." ameongeza.
Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Annalena Baerbock amesema mwaka wa 80 wa Umoja wa Mataifa unakuja katika hatua ya mabadiliko. "Lazima tuchague njia sahihi; ili kuionyesha dunia kuwa tunaweza kuwa bora zaidi pamoja," amesema, akiongeza kuwa "Pamoja ni bora zaidi" ni zaidi ya kauli mbiu, lakini ukweli uliopatikana kwa bidii kubwa na kudhamiria kwa miaka 80 ijayo.
Wazungumzaji watatu -- Rais wa zamani wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf, Waziri Mkuu wa zamani wa Norway Gro Harlem Brundtland, na mwanahabari mashuhuri Maria Ressa -- wametoa wito wa kuchukua hatua juu ya amani, maendeleo endelevu, na uadilifu wa habari.
Sirleaf ameonya kuwa "maadhimisho bila udhati ni yasiyo na maana" na kutoa wito wa dhamira za kulinda raia na kuwezesha vijana.
Brundtland amesema asilimia zaidi ya 80 ya Malengo ya Maendeleo Endelevu yako nje ya kufikiwa, akisisitiza kuwa Umoja wa Mataifa bado ni muhimu kwa tabianchi na usawa wa kijinsia.
Ressa ameelezea "dhoruba kuu ya habari" inayoendeshwa na habari potoshi na akili mnemba, akiuita uadilifu wa habari "mama wa vita vyote."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




