

Lugha Nyingine
Rais Xi aongoza ujumbe wa mamlaka kuu za China kwenda Urumqi kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 70 ya Mkoa wa Xinjiang (4)
URUMQ - Rais wa China Xi Jinping akiongoza ujumbe wa maofisa waandamizi wa Chama na Serikali Kuu amewasili Urumqi, mji mkuu wa Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang jana Jumanne mchana kushiriki kwenye shughuli za kuadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa kwa mkoa huo unaojiendesha, na hii ni mara ya kwanza kufanya shughuli kama hizo katika historia ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na China.
Majira ya saa 8:20 mchana, ndege maalum iliyombeba Rais Xi ilitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Urumqi Tianshan. Alitoka nje ya chumba cha abiria na kupungia mkono umati wa watu waliokuwa wanamkaribisha kwa furaha.
Wakati akishuka kutoka kwenye ngazi za ndege, Rais Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) alipokea maua kutoka kwa watoto na alikaribishwa na watu wa makabila mbalimbali walioimba nyimbo na kucheza ngoma.
Watu waliolijipanga kwenye kando za barabara huko Urumqi, wakipeperusha bendera nyekundu za Taifa la China, kuukaribisha msafara wake huku Rais Xi akiwapungia watu mkono kupitia dirisha la gari.
Rais Xi ameambatana na Wang Huning, mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China ambaye ni mkuu wa ujumbe wa Serikali kuu ya China, vilevile Cai Qi, mkurugenzi wa Ofisi Kuu ya Kamati Kuu ya CPC. Wang na Cai wote ni wajumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma