Rais Xi Jinping atoa wito wa kufanya juhudi za pamoja za kuijenga vizuri zaidi Xinjiang inayopendeza (7)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 24, 2025
Rais Xi Jinping atoa wito wa kufanya juhudi za pamoja za kuijenga vizuri zaidi Xinjiang inayopendeza
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akiwa kwenye picha pamoja na makada waliotoka sehemu nyingine nchini China wanaofanya kazi mkoani Xinjiang katika Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, kaskazini-magharibi mwa China, mjini Urumqi, mji mkuu wa mkoa huo, Septemba 23, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)

URUMQI - Rais wa China Xi Jinping ametoa wito wa kufanya juhudi za pamoja za kuijenga vizuri zaidi Xinjiang inayopendeza katika mchakato wa ujenzi wa mambo ya kisasa wa China, alipokutana na wajumbe kutoka makabila na sekta mbalimbali jana Jumanne katika Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, kaskazini magharibi mwa China.

Rais Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), aliwasili Urumqi, mji mkuu wa Xinjiang, mapema siku hiyo ya Jumanne kuhudhuria shughuli za kuadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa kwa mkoa huo.

Kwa niaba ya Kamati Kuu ya CPC, ametoa salamu za dhati na salamu za upendo za kutakia kila la kheri kwa watu wa makabila mbalimbali mkoani humo Xinjiang.

Rais Xi pia amekutana kwa nyakati tofauti na maofisa wa mkoa huo, viongozi wa Kikosi cha Uzalishaji na Ujenzi cha Xinjiang, makada waliotoka sehemu nyingine nchini China wanaofanya kazi mkoani Xinjiang, wafanyakazi wa mahakama, maofisa wa polisi, pamoja na wadau wazalendo wa sekta ya dini. Rais Xi pia amekutana na maofisa wa jeshi wenye vyeo vya makanali na zaidi, pamoja na watu wa mfano wa kuigwa wa mashinani na wafanyakazi wa kiraia kutoka kwenye majeshi yaliyoko Urumqi. Ametoa salamu za upendo kwa wanajeshi wote wa Xinjiang akiwa kwa niaba ya Kamati Kuu ya CPC na CMC.

Maofisa waandamizi, akiwemo Wang Huning na Cai Qi, walihudhuria mikutano hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha