Watu washerehekea Nchi za Magharibi kutambua nchi ya Palestina katika Ukingo wa Magharibi (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 24, 2025
Watu washerehekea Nchi za Magharibi kutambua nchi ya Palestina katika Ukingo wa Magharibi
Wapalestina wakisherehekea kwa kushika bendera za Palestina kwenye maandamano katika mji wa Ukingo wa Magharibi wa Nablus, Septemba 23, 2025. (Picha na Nidal Eshtayeh/Xinhua)

RAMALLAH - Maandamano yamefanyika katika miji kadhaa ya Ukingo wa Magharibi jana Jumanne kusherehekea nchi za Magharibi kutambua nchi ya Palestina na kuonyesha mshikamano na watu wa Ukanda wa Gaza ambapo mamia ya Wapalestina, pamoja na wanaharakati wa kimataifa, wameshiriki katika maandamano hayo kwenye uwanja wa Al-Manara mjini Ramallah huku watu wakipeperusha bendera za Palestina, ikiambatana na sauti za kaulimbiu na muziki.

Bango lililokuwa limetundikwa juu lilisomeka kuwa tukio hili ni kwa ajili ya "kuunga mkono Gaza na wafungwa na kukataa vita vya maangamizi," na "kuthamini misimamo ya kimataifa inayounga mkono haki ya watu wetu ya uhuru."

Sabri Saidam, mjumbe wa kamati kuu ya Fatah, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kwenye maandamano hayo kwamba ni "siku ya shangwe kwa Wapalestina" na Wapalestina "wanaheshimu" nchi zinazounga mkono Palestina.

Kumaliza vita katika Gaza ni "kipaumbele," Saidam amesema. "Inabidi tushirikiane. Inabidi tusimamishe vita. Hiyo ni ya jambo la haraka. Kisha tushiriki katika ujenzi wa Gaza... Tuna kazi nyingi mbele yetu, lakini tuko na dhamira. Hayo ni maisha yetu ya baadaye. Huu ni utambulisho wetu. Hiyo ni heshima yetu." 

Luisa Morgantini, makamu rais wa zamani wa Bunge la Ulaya, amekuwa safarini kwenye Ukingo wa Magharibi, na pia alishiriki kwenye maandamano hayo. Ameliambia Xinhua kwamba utambuzi wa Ulaya ni "hatua muhimu".

"Tunahisi kwamba Palestina lazima iwe huru. Wapalestina wanapaswa kuchagua wenyewe kile wanachotaka... Wana uwezo wa kujenga, kujenga taifa lao wenyewe." Morgantini amesema.

Katika mahojiano hayo, Morgantini amezihimiza nchi za Magharibi kufanya zaidi kwa ajili ya "uhuru na kujitawala kwa Palestina."

Ufaransa, Uingereza, Ureno, Australia, na Canada ni miongoni mwa nchi za Magharibi ambayo hivi karibuni yamelitambua nchi ya Palestina katika kuunga mkono suluhisho la nchi mbili. Hadi sasa, nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zaidi ya 150 zimeitambua Palestina.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha