Lugha Nyingine
UNGA yaanza mjadala kushughulikia masuala ya kimataifa (4)
UMOJA WA MATAIFA - Wawakilishi kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, wakiwemo wakuu wa nchi na serikali wapatao 150, watapeana zamu katika jukwaa la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) kutoa hotuba kuhusu masuala ya kimataifa wakati wa mjadala wa jumla wa UNGA ulioanza rasmi jana Jumanne kwa viongozi mbalimbali wakiwemo Rais Luiz Inacio Lula da Silva wa Brazil, Rais Donald Trump wa Marekani na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.
Katika hotuba yake kwa UNGA, Guterres amesema dunia "imeingia katika zama ya uvurugaji wa kiholela na mateso yasiyokoma kwa binadamu," huku kanuni za Umoja wa Mataifa "zinashambuliwa" na nguzo za amani na maendeleo "zikiyumbishwa chini ya uzito wa dharau, ukosefu wa usawa na kutojali."
Akisema kuwa dunia inazidi kuwa yenye ncha nyingi, Guterres amesema uwepo wa dunia yenye ncha nyingi bila taasisi zenye ufanisi za kimataifa husababisha machafuko.
"Machaguo tunayokabiliana nayo si sehemu ya mdahalo wa kiitikadi. Ni masuala ya maisha na kifo kwa mamilioni ya watu," amesema, akiongeza kuwa amani iliyokita mizizi katika sheria za kimataifa ni wajibu wa kwanza wa binadamu.
Akisisitiza kwamba "haki za binadamu si pambo la amani -- ni msingi wake," amesema haki hizo -- kijamii, kiuchumi, kisiasa, kiraia na kitamaduni -- ni za wote duniani, hazina mbadala na zinategemeana.
Amesema, na ingawa "tuna suluhu na zana," mpango wa kufanikisha hayo kupitia dira ya pamoja ya Malengo ya Maendeleo Endelevu yanahitaji ufadhili, lakini kupunguza misaada kunasababisha uharibifu mkubwa.
Mjadala huo utahitimishwa Septemba 29. Wawakilishi na wakuu wa nchi na serikali pia watahudhuria mikutano mbalimbali ya ngazi ya juu na kufanya mikutano ya pande mbili wakati wa Wiki ya Ngazi ya Juu iliyoanza Septemba 22 na itaendelea hadi Septemba 30.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




