Reli ya Quzhou-Ningde nchini China kuadhimisha miaka 5 tangu kufunguliwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 25, 2025
Reli ya Quzhou-Ningde nchini China kuadhimisha miaka 5 tangu kufunguliwa
Picha iliyopigwa Septemba 24, 2025 ikionyesha abiria wakipanda na kushuka kwenye treni iliyosimama kwenye Stesheni ya Zhenghe ya Reli ya Quzhou-Ningde katika Wilaya ya Zhenghe, Mji wa Nanping, Mkoa wa Fujian, kusini-mashariki mwa China. (Xinhua/Lin Shanchuan)

Reli ya Quzhou-Ningde, ambayo inaunganisha maeneo yaliyoendelea kiuchumi katika mkoa wa Zhejiang mashariki mwa China na maeneo ya ndani ya milima ya Mkoa wa Fujian, kusini mashariki mwa China ilianza kufanya kazi yake rasmi mwezi Septemba, 2020, na inakaribia kutimiza miaka 5 tangu kufunguliwa kwake.

Reli hiyo imekuwa ikisaidia kusafirisha bidhaa kama vile nguo na chai kutoka Fujian kwenda duniani, ikiongeza ustawi kwenye maeneo ya milimani kaskazini mashariki mwa mkoa huo wa Fujian.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha