Timu ya watu wa kujitolea Kaskazini Mashariki mwa China yajitahidi kulinda wanyamapori katika eneo la Mto Songhua (8)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 22, 2025
Timu ya watu wa kujitolea Kaskazini Mashariki mwa China yajitahidi kulinda wanyamapori katika eneo la Mto Songhua
Watu wa kujitolea wakifanya shughuli ya kuhimiza ulinzi wa ndege mjini Harbin, Mkoa wa Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China, Oktoba 25, 2020. (Picha na Zhang Shu/Xinhua)

Timu inayoundwa na watu 60 wa kujitolea ya kuwalinda wanyamapori ya Harbin imefanya juhudi za muda mrefu za kuhifadhi mazingira ya ikolojia katika eneo la mtiririko wa Mto Songhua, katika Mkoa wa Heilongjiang, kaskazini-mashariki mwa China.

Katika muda wa miaka saba iliyopita, timu hiyo imefanya doria kwenye eneo la kilomita takriban 30,000 na kuripoti habari karibu 100 kuhusu uwindaji haramu kwa ofisi husika.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha