Njia maalum kando ya Mfereji Mkuu wa China mkoani Hebei yasukuma mbele maendeleo ya mkoa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 04, 2025
Njia maalum kando ya Mfereji Mkuu wa China mkoani Hebei yasukuma mbele maendeleo ya mkoa
Watu wakitembelea Mnara wa Nanchuan kando ya Mfereji Mkuu wa China katika Eneo la Yunhe la Mji Cangzhou, Mkoa wa Hebei, kaskazini mwa China, Oktoba 29, 2025. (Xinhua/Mu Yu)

CANGZHOU - Mfereji Mkuu wa China, unaounganisha Mji wa Beijing kaskazini mwa China na Mji wa Hangzhou mashariki mwa China, una historia ya miaka zaidi ya 2,500 na unajulikana kama njia ndefu zaidi ya maji iliyojengwa na binadamu duniani.

Njia maalum ya kulinda kingo za Mfereji Mkuu huo imejengwa katika sehemu ya Mji Cangzhou ya kando za Mfereji Mkuu huo katika Mkoa wa Hebei, kaskazini mwa China, ikienea urefu wa kilomita 308 na kupita vijiji zaidi ya 300 katika sehemu mbalimbali za mji huo. Njia hiyo inaunganisha mandhari ya mazingira ya asili, maeneo ya mabaki ya kale ya kihistoria na kitamaduni, na vivutio vya kitamaduni kando ya Mfereji Mkuu.

Aidha, bustani za mada mbalimbali na miundombinu husika zaidi ya kumi vimejengwa upande wa njia hiyo, na kuleta nafasi ya shughuli mbalimbali za utalii, mapumziko, mazoezi ya kujenga mwili, na shughuli za burudani.

Njia hiyo si tu imenufaisha wenyeji wa huko bali pia imehimiza mafungamano ya maeneo mbalimbali ya mkoa huo na kuleta nguvu hai kwa maendeleo ya uchumi na jamii ya mkoa huo.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha