Barabara Kuu ya Kitaifa ya G331 ya China yaleta nguvu hai katika eneo la kando za barabara (7)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 13, 2025
Barabara Kuu ya Kitaifa ya G331 ya China yaleta nguvu hai katika eneo la kando za barabara
Picha hii iliyopigwa Oktoba 12, 2025 ikionyesha Daraja la Hunjiangkou, sehemu ya kuanzia ya sehemu ya Jilin ya barabara kuu ya kitaifa ya G331, kwenye mpaka kati ya Mji wa Dandong wa Mkoa wa Liaoning na Mji wa Tonghua wa Mkoa wa Jilin, kaskazini mashariki mwa China. (Xinhua/Wu Qinghao)

Barabara kuu ya kitaifa ya G331, yenye urefu wa kilomita 9,333 kwa jumla kutoka Mji wa Dandong wa Mkoa wa Liaoning, kaskazini mashariki mwa China hadi Mji Altay wa Mkoa Unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, kaskazini magharibi mwa China, ni barabara kuu ya pili kwa urefu zaidi nchini China. Barabara hiyo inapita mikoa sita ya kaskazini mashariki, kaskazini na kaskazini magharibi mwa China, na inasifiwa kuwa "barabara inayopendeza zaidi ya maeneo ya mpakani".

Barabara hiyo inaunganisha vijiji vingi na maeneo yenye vivutio vya utalii katika sehemu za mikoa ya Liaoning na Jilin, na imeleta nguvu hai na maendeleo katika maeneo hayo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha