Mkutano na wasomaji wa China na Kenya wa kitabu cha Xi Jinping cha “Utawala wa China” wafanyika Nairobi (2)

(CRI Online) Desemba 02, 2025
Mkutano na wasomaji wa China na Kenya wa kitabu cha Xi Jinping cha “Utawala wa China” wafanyika Nairobi
(Picha/Xinhua)

Nairobi, Desemba, 1--Habari kutoka Shirika la Habari la China Xinhua zinasema kuwa, Mkutano na wasomaji wa China na Kenya kuhusu kitabu cha Xi Jinping cha "Utawala wa China" ulifanyika Nairobi, mji mkuu wa Kenya. Mkutano huo uliandaliwa kwa pamoja na Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China, Shirika la mawasiliano ya kimataifa la China (CICG), na Ubalozi wa China nchini Kenya. Takribani watu 200 kutoka sekta mbalimbali za China na Kenya walihudhuria mkutano huo.

Wasomaji wa China na Kenya waliohudhuria mkutano huo wamesema kuwa juzuu ya tano ya kitabu cha Xi Jinping cha “Utawala wa China” pamoja na juzuu ya kwanza hadi juzuu ya nne zinaelezea maudhui makuu na mfumo wa kisayansi wa Fikra ya Xi Jinping kuhusu Ujamaa wenye umaalumu wa China katika zama mpya, na kitabu cha Xi Jinping cha “Utawala wa China” kinasaidia jumuiya ya kimataifa kuelewa kwa undani zaidi mafanikio ya China katika ujenzi wa mambo ya kisasa wa China, pamoja na umuhimu wake kwa dunia. Pia wamesema kuna umuhimu mkubwa kwa kubadilishana mawazo kuhusu uzoefu wa utawala wa nchi kati ya China na Kenya, na China na Afrika, na kufikia maoni ya pamoja ya Nchi za Kusini mwa Dunia kuhusu maendeleo, pamoja na kujenga Jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

Katibu Mkuu wa Chama cha UDA cha Kenya, Hassan Omar Hassan, amesema kuwa chini ya uongozi wa Rais Xi Jinping, China imepata mafanikio makubwa ya maendeleo, huku uchumi na jamii yake vikikua kwa kasi na kiwango cha maisha ya watu kimeinuka kidhahiri. Amesema kuwa Kitabu cha Xi Jinping cha “Utawala wa China” si mkusanyiko tu wa hotuba, bali ni ujuzi na falsafa, na maelezo muhimu yaliyomo kuhusu uchumi, kupunguza umaskini, sayansi na teknolojia, usalama na mambo mengine yanatoa dira ya kifikra kwa Kenya wakati wa kukabiliana na changamoto. Kenya inapenda kubadilishana mawazo zaidi na China kuhusu uzoefu wa maendeleo ya ujenzi wa mambo ya kisasa, ili kuhimiza ustawi kwa pamoja na kuleta manufaa zaidi kwa watu wa nchi hizo mbili.

Naibu mkuu wa Idara ya Uenezi ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkurugenzi wa Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China Bw. Mo Gaoyi, amesema, kitabu cha Xi Jinping cha “Utawala wa China” ni matokeo mapya ya kuufanya Umarx uendane na hali halisi ya China, kikionyesha maudhui makuu na mfumo wa kisayansi wa Fikra ya Xi Jinping kuhusu Ujamaa wenye umaalumu wa China katika zama mpya. Kinaonesha mafanikio ya kihistoria ya njia ya ujenzi wa mambo ya kisasa ya China, njia yake ya kujiendeleza, na sifa yake kuu, na kinatoa hekima na mpango wa China vinavyoweza kuigwa kwa Nchi za Kusini mwa Dunia katika kujenga mambo yao ya kisasa kwa pamoja.

Ameongeza kuwa, China na Kenya zitaadhimisha miaka 62 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati yao, na katika miaka hiyo iliyopita nchi hizo mbili zimekuwa zikishirikiana na kusaidiana, na kuwa marafiki wanaoaminiana kisiasa na washirika wa kiuchumi wanaonufaishana. China inapenda kuimarisha mshikamano na ushirikiano na nchi za Afrika ikiwemo Kenya, kutekeleza kwa pamoja mapendekezo makubwa manne kwa dunia, kujenga kwa pamoja “Ukanda Mmoja, Njia Moja” kwa sifa bora, na kutekeleza kwa vitendo Hatua 10 za washirika wa maendeleo ya ujenzi wa mambo ya kisasa, kutoa fursa zaidi kwa Afrika kupitia maendeleo mapya ya ujenzi wa mambo ya kisasa ya China, na kuandika ukurasa mpya wa jumuiya ya hali zote ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya.

Waziri wa Upashanaji Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Kidijitali wa Kenya TBC, William Kabogo Gitau, amesema kuwa China imehimiza mchakato wa ustaarabu wa dunia katika wakati wa kusukuma mbele mchakato wake wa ujenzi wa mambo ya kisasa, na mafanikio mbalimbali ya China na wazo wa utawala vinaendana na malengo ya mageuzi ya Kenya. Amesema kuwa maudhui ya vitabu vya juzuu mbalimbali za “Utawala wa China” yanahusisha mambo mengi mbalimbali, na wazo la maendeleo linaloonekana kwenye maelezo ya vitabu linatoa ushauri muhimu kwa Kenya katika kufanya utafiti kwenye njia yake ya ujenzi wa mambo ya kisasa. Juzuu ya tano ya kitabu hicho iliyochapishwa hivi karibuni itasaidia wasomaji wa Kenya kufahamu hali ya maendeleo ya China ya zama za hivi sasa, na kuongeza maelewano kati ya China na Kenya.

Katika shughuli husika ya mkutano huo, wageni waheshimiwa wa Kenya wamezawadiwa toleo la Kiingereza la juzuu ya tano ya kitabu cha Xi Jinping cha "Utawala wa China". Wataalamu na wasomi waliohudhuria mkutano huo, wamebadilishana mawazo kuhusu mada mbalimbali zikiwemo uzoefu wa utawala wa nchi wa China na Kenya, ujenzi wa pamoja wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", ushirikiano kati ya China na Afrika, kutokomeza umaskini, na mawasiliano ya kitamaduni.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha