Manowari ya kombora la kuongozwa ya Vietnam yafanya ziara katika Mji wa Qingdao mashariki mwa China (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 02, 2025
Manowari ya kombora la kuongozwa ya Vietnam yafanya ziara katika Mji wa Qingdao mashariki mwa China
Manowari ya ulinzi ya Vietnam ya Tran Hung Dao ikiwasili katika bandari ya kikosi cha majini huko Qingdao, Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China, Desemba 1, 2025. (Picha na Wang Liantao/Xinhua)

QINGDAO - Manowari ya kombora la kuongozwa ya Vietnam ya Tran Hung Dao imewasili kwenye bandari ya kikosi cha majini huko Qingdao, Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China jana Jumatatu, ikiwa ni mwanzo wa ziara ya siku nne ya manowari hiyo, ambapo vikosi cha majini vya majeshi ya China na Vietnam vitatembelea kwenye manowari, kufanya mapokezi kwenye sitaha, kufanya mawasiliano ya kiutamaduni na kufanya mazoezi kwa pamoja.

Habari zinasema kuwa, ziara hiyo inalenga kuongeza maelewano kati ya vikosi hivyo vya majini vya majeshi ya pande hizo mbili, na kuzidisha urafiki kati ya nchi hizo mbili.

Manowari hiyo ina uwezo kamili wa uzito wa meli ikiwa na mzigo tani 2,100 na kasi ya juu ya knots zaidi ya 29. Inaweza kubeba helikopta moja ya kupambana na manowari.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha