Lugha Nyingine
Shughuli za Utalii zastawi katika Eneo la Liujiang, Mkoa wa Guangxi, kusini mwa China (2)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 04, 2025
![]() |
| Watalii wakitembelea Kijiji cha Baipeng la Eneo la Liujiang la Mji wa Liuzhou, Mkoa Unaojiendesha wa Kabila Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China, Desemba 2, 2025. (Xinhua/Huang Xiaobang) |
Katika miaka ya hivi karibuni, Eneo la Liujiang la Mji wa Liuzhou katika Mkoa Unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China limeendeleza zaidi shughuli zake za utalii kwa kutegemea viwanda vyake vya vijijini vinavyostawi na uchumi wake wa kilimo unaojaa nguvu hai.
Katika robo tatu za kwanza za mwaka huu, eneo hilo la Liujiang lilipokea watalii kwa jumla ya zaidi ya mara milioni 5.9975, ikiwa ni ongezeko la asilimia 11.16 kuliko lile la kipindi kama hicho mwaka jana, na mapato yanayotokana na shughuli za utalii yamefikia yuan bilioni 6.006 (dola za Marekani milioni 850.26), yakiongezeka kwa asilimia 9.91 kuliko lile la kipindi kama hicho mwaka jana.
(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




