Lugha Nyingine
Magulio ya wakulima yaanza katika Mji mdogo wa Qiantan, Mkoa wa Zhejiang, China (7)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 08, 2025
![]() |
| Watu wakichagua bidhaa kwenye magulio ya wakulima katika Mji mdogo wa Qiantan wa Mji wa Jiande, Mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China, Desemba 6, 2025. (Xinhua/Xu Yu) |
Magulio ya wakulima yameanza katika Mji mdogo wa Qiantan wa Mji wa Jiande, Mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China juzi Jumamosi. Mabanda zaidi ya 300 yamepangwa kwenye njia ya watembea kwa miguu kando ya mto yenye urefu wa kilomita karibu mbili, huku mahitaji mbalimbali ya kila siku, bidhaa za kilimo, vitafunio vya kienyeji, midoli ya watoto na zaidi vikionyeshwa kwenye magulio.
Yakiwa ni shughuli moja ya kufurahisha zaidi inayofanyika mwishoni mwa mwaka katika eneo hilo, magulio hayo ya wakulima yanayoendelea pia yanahusisha maonesho ya kitamaduni na soko la kuajiri watu wenye vipaji.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




