Mfumo wa umwagiliaji maji wa Dujiangyan uliojengwa Mwaka 256 KK Chengdu, China wavutia watalii

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 08, 2025
Mfumo wa umwagiliaji maji wa Dujiangyan uliojengwa Mwaka 256 KK Chengdu, China wavutia watalii
Watu wakifahamishwa kuhusu mfumo wa umwagiliaji maji wa Dujiangyan kwenye eneo la vivutio vya utalii la Dujiangyan la Chengdu, Mkoa wa Sichuan, kusini magharibi mwa China, Novemba 30, 2025. (Xinhua/Xu Bingjie)

Mfumo wa umwagiliaji maji wa Dujiangyan wenye sifa ya uchepushaji wa maji usio wa mabwawa, ulijengwa mwaka 256 KK na ni mradi wa kale zaidi, wa pekee uliobaki wa kuhifadhi maji duniani, ambao umestahimili majaribu ya maafa kama vile mafuriko na matetemeko ya ardhi, na bado unatumika hadi leo.

Ukingo wa maji wenye umbo la "mdomo wa samaki" unagawanya Mto Minjiang kuwa mkondo wa ndani wa umwagiliaji maji na mkondo wa nje kwa ajili ya kutoa maji ya mafuriko.

Mfumo huo wa umwagiliaji uliorodheshwa kuwa mali ya Urithi wa Utamaduni wa Dunia na Umoja wa Mataifa mwezi wa Novemba mwaka 2000, na uliorodheshwa kuwa mali ya Urithi wa Uhandisi wa Umwagiliaji Duniani mwezi wa Agosti mwaka 2018.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha