Mizigo iliyopitishwa na Bandari ya Qingdao ya China mwaka 2025 yazidi tani milioni 700

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 09, 2025
Mizigo iliyopitishwa na Bandari ya Qingdao ya China mwaka 2025 yazidi tani milioni 700
Picha iliyopigwa Desemba 8, 2025 ikionyesha mandhari ya Bandari ya Qingdao katika Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China. (Xinhua/Li Ziheng)

Upitishaji wa mizigo wa Bandari ya Qingdao katika Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China kwa mwaka 2025 ulizidi tani milioni 700 hadi jana Jumatatu, ukifikia hatua hii siku 15 mapema ikilinganishwa na mwaka 2024.

Bandari hiyo ya Qingdao imeendelea kupanua mtandao wake wa kimataifa wa usafirishaji, ikiwa na njia karibu 240 zinazounganisha bandari zaidi ya 700 katika nchi na maeneo zaidi ya 180 duniani kote.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha