Sehemu ya Nanping ya Barabara ya mwendo kasi ya Shaxian-Nanping, China yazinduliwa kwa usafiri wa magari

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 10, 2025
Sehemu ya Nanping ya Barabara ya mwendo kasi ya Shaxian-Nanping, China yazinduliwa kwa usafiri wa magari
Picha iliyopigwa Desemba 9, 2025 ikionyesha daraja kubwa la Barabara ya mwendo kasi ya Shaxian-Nanping, Mkoa wa Fujian, kusini mashariki mwa China. (Picha na Yin Ting/Xinhua)

Ujenzi wa Sehemu ya Nanping ya Barabara ya mwendo kasi ya Shaxian-Nanping katika Mkoa wa Fujian, kusini mashariki mwa China umekamilika na kuzinduliwa kwa usafiri wa magari jana Jumanne, ikimaanisha kuanza kufanya kazi kwa barabara hiyo ya mwendo kasi.

Barabara hiyo ya Shaxian-Nanping inaunganisha Wilaya ya Shaxian ya Mji wa Sanming na Mji wa Nanping mkoani Fujian. Baada ya barabara hiyo ya mwendo kasi kufunguliwa kwa usafiri wa magari, muda wa kusafiri kutoka Shaxian hadi Mlima Wuyishan wa Nanping umefupishwa na kuwa muda wa saa 1.5.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha