Mtandao wa ushirikiano kuhusu utafiti wa mambo ya kibinadamu kati ya China na Afrika waanzishwa

(CRI Online) Desemba 11, 2025
Mtandao wa ushirikiano kuhusu utafiti wa mambo ya kibinadamu kati ya China na Afrika waanzishwa
(Picha/Xinhua)

Kongamano la “Utekelezaji wa mapendekezo manne ya dunia, kukuza ushirikiano wa mambo ya haki za binadamu kati ya China na Afrika”, na hafla ya uzinduzi wa mtandao wa ushirikiano wa jopo la washauri bingwa wa utafiti wa mambo ya kibinadamu kati ya China na Afrika vimefanyika jana huko Jinhua, mkoani Zhejiang, China.

Naibu mkurugenzi wa Taasisi ya haki za binadamu ya China Shen Yongxiang amesema, uzinduzi wa mtandao huo una umuhimu mkubwa, na kwamba anatarajia utaangazia masuala mapya ya haki za binadamu kufuatia maendeleo na usalama wa dunia, na changamoto mpya za ulinzi wa haki za binadamu zinazokabili China na Afrika.

Pia kutoa matokeo ya utafiti yanayotupia macho mbali, yenye kiujenzi na yanayoweza kutekelezwa, ili kupaza sauti za China na Afrika katika kuhimiza mambo ya haki za binadamu na kupata maendeleo ya pamoja.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha