Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping wa China atoa hotuba muhimu kwenye Mkutano wa Kamati Kuu ya CPC kuhusu kazi ya uchumi
Mkutano wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kuhusu kazi ya uchumi umefanyika mjini Beijing kuanzia tarehe 10 hadi tarehe 11 Desemba.
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC, amehudhuria mkutano huo na kutoa hotuba muhimu, akifanya majumuisho kuhusu kazi ya uchumi ya mwaka 2025, kuchambua hali ya uchumi kwa hivi sasa, na kutoa maelekezo kuhusu kazi ya uchumi ya mwaka 2026.
Mkutano huo umesema Kamati Kuu ya CPC ambayo Komredi Xi Jinping akiwa kiini chake imewaongoza watu wa China kushinda taabu na changamoto mbalimbali, kutekeleza sera za jumla za kuhimiza juhudi zaidi, na malengo makuu ya maendeleo ya uchumi na jamii yanatarajiwa kutimizwa kwa mafanikio.
Mkutano huo umesisitiza kuwa ili kufanya vizuri kazi za uchumi mwaka ujao, ni muhimu kufuata fikra ya Xi Jinping ya Ujamaa wenye Umaalum wa China katika Zama Mpya, kutekeleza kikamilifu mawazo mapya ya maendeleo katika sekta zote, kuongeza kasi ya kuunda muundo mpya wa maendeleo. Pia kuweka mkazo katika kukuza maendeleo yenye sifa bora, kushikilia kanuni za jumla za kufanya kazi na kutafuta maendeleo kwa hatua madhubuti, na kuratibu ipasavyo kazi za uchumi wa ndani na mambo ya kiuchumi na kibiashara ya kimataifa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




