Bustani kubwa zaidi duniani ya mandhari ya barafu na theluji kufunguliwa kaskazini mashariki mwa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 15, 2025

Picha iliyopigwa Februari 25, 2025 ikionyesha watalii wakitembelea Bustani ya Dunia ya Barafu na Theluji ya Harbin katika Mkoa wa Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China. (Xinhua/Wang Song)

Picha iliyopigwa Februari 25, 2025 ikionyesha watalii wakitembelea Bustani ya Dunia ya Barafu na Theluji ya Harbin katika Mkoa wa Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China. (Xinhua/Wang Song)

HARBIN – Maonyesho ya 27 ya Dunia ya Barafu na Theluji ya Harbin, ambayo ni bustani kubwa zaidi duniani ya mandhari ya barafu na theluji, itafunguliwa rasmi kwa umma kuanza kuitembelea Desemba 17 katika "mji wa barafu" wa China, Harbin, mji mkuu wa mkoa wa kaskazini mashariki wa Heilongjiang.

Bustani hiyo ina eneo la urefu wa mita za mraba milioni 1.2 na inajengwa kwa kutumia mita za ujazo 400,000 za barafu na theluji chini ya kaulimbiu ya mwaka huu ya "Barafu na Theluji, Dunia ya Simulizi ya Ajabu."

Bustani hiyo imegawanywa kuwa na njia kuu tatu za kutazama mandhari, shughuli kubwa za utalii kuhusu mada maalum, jukwaa la nje na majengo yanayojazwa hewa yenye ukubwa wa mita za mraba 5,000. Majengo ya bustani hiyo mpya imeonesha hali ya mafungamano ya mambo ya kiteknolojia kama vile taa za teknolojia za kisasa na kuchangamana na kujaribu vifaa vyenye kutumia AI.

Katika bustani hiyo, zitafanyika shughuli mbalimbali zikiwemo hafla ya ufunguzi wa Tamasha la Kimataifa la Barafu na Theluji la Harbin, mashindano ya kimataifa ya sanaa za michongo ya barafu, mechi za mpira wa miguu kwenye theluji na mashindano ya hoki ya kwenye barafu, pamoja na tamasha la muziki la usiku wa Kuamkia Mwaka Mpya.

Kwa mujibu wa waandaaji, tiketi za kuingia kwenye bustani hiyo zinaweza kupatikana kwa ununuzi wa mapema kupitia akaunti rasmi ya mtandao wa WeChat ya bustani hiyo ya Dunia ya Barafu na Theluji ya Harbin na njia nyingine za mtandaoni zikiwemo Meituan na Alipay. Wamefafanua kuwa, bei ya ofa ya yuan 298 (dola za Marekani takribani 42) kwa kila tiketi ya mtu mzima itaanza Desemba 17 hadi 23, kabla ya kurejea kwenye bei ya kawaida ya yuan 328.

Zaidi ya Bustani ya Dunia ya Barafu na Theluji, Harbin inatangaza maeneo mengine mawili makubwa ya utalii wa majira ya baridi: Maonyesho ya Theluji ya Kisiwa cha Jua yenye ukubwa wa mita za mraba milioni 1.5 na Kanivali ya Barafu na Theluji kando ya Mto Songhua ulioganda, ambapo itaonekana sanaa za michongo ya theluji 260 na miradi 60 ya burudani kwenye barafu na theluji.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha