Lugha Nyingine
Benki za kigeni zatumia fursa katika biashara za nje za kampuni za China

Picha hii iliyopigwa Desemba 13, 2025 ikionyesha mandhari ya theluji kwenye majengo marefu mjini Beijing, China. (Xinhua/Chen Yehua)
BEIJING - Tawi la Beijing la Mamlaka ya Taifa ya Udhibiti na Usimamizi wa Mambo ya Fedha ya China limesema kwamba Benki za kigeni mjini Beijing zimeunga mkono kampuni za viwanda vya China katika kufanya biashara nje ya nchi, zikinufaika pamoja na faida za ukuaji wa kampuni na viwanda vya China.
Tawi hilo limesema jana Jumapili kuwa, mwaka 2024, benki hizo zilitoa msaada wa mambo ya fedha kwa biashara za nje za kampuni 14,900 za China, ambapo jumla ya fedha hizo ikifikia yuan trilioni 1.24 (dola za Marekani takribani bilioni 175.54).
"Kwa sasa, benki 48 za kigeni kutoka nchi na maeneo 17 zimeanzisha matawi ya uendeshaji mjini Beijing." limesema.
Tawi hilo limeeleza kuwa, mji wa Beijing utaendelea kutumika kama uwanja wa majaribio ya mageuzi ya mambo ya fedha na kuunga mkono maendeleo ya benki hizo za kigeni katika kuzoea matarajio, desturi na vizuizi katika sehemu zilipo na kuendeshwa kwa utaaluma zaidi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



