Lugha Nyingine
Kongamano juu ya kudhibiti hali ya kuenea kwa jangwa latoa wito wa kuimarisha ushirikiano kati ya China na Afrika
Maofisa na wataalam kutoka China na Afrika juzi Jumapili walitoa wito wa ushirikiano imara zaidi wa kisayansi na kiteknolojia ili kukabiliana na hali ya kuenea kwa jangwa na kuvia kwa ardhi, wakihimiza uratibu wa karibu zaidi kwa ajili ya kusukuma mbele Mpango wa Ukuta Mkuu wa Kijani wa Afrika (Great Green Wall).
Wito huo umetolewa kwenye Kongamano la nne la Kimataifa la Jangwa la Taklamakan, lililofanyika Nouakchott nchini Mauritania, ambapo washiriki wamesisitiza kuwa hali ya kuenea kwa jangwa bado ni changamoto ya kimataifa inayohitaji hatua za pamoja na mabadilishano ya uzoefu.
Naibu Mkuu wa Taasisi ya Ikolojia na Jiografia ya Xinjiang iliyo chini ya Akademia ya Sayansi ya China, Bw. Duan Weili, amesema China imeendeleza mbinu maalum ya kupambana na hali ya kuenea kwa jangwa kupitia juhudi endelevu za zaidi ya miaka 70, ikiunganisha usimamizi wa kisayansi, hatua jumuishi na urejeshaji wa ikolojia unaozingatia ustawi wa maisha ya watu.
Bw. Duan amesema China iko tayari kuimarisha ushirikiano na nchi za Afrika ili kuwezesha teknolojia za kudhibiti jangwa kutumika na kufanya kazi kwa ufanisi katika nchi hizo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



