Lugha Nyingine
Walinzi wawili wa amani wa Umoja wa Mataifa wajeruhiwa katika shambulizi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati
Walinzi wawili wa amani wa Umoja wa Mataifa wamejeruhiwa wakati msafara wa kusafirisha vifaa wa Ujumbe wa Kuleta Utulivu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA) uliposhambuliwa jana Jumatatu na watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa kundi lenye silaha katika Mkoa wa Haut-Mbomou.
Naibu Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Farhan Haq, amesema kwenye mkutano wa kila siku na waandishi wa habari kuwa walinzi hao wawili wa amani wanatoka Nepal na wamehamishiwa katika mji mkuu wa nchi hiyo wa Bangui ili kupata matibabu.
Mkuu wa MINUSCA Bw. Valentine Rugwabiza, ameelezea wasiwasi wake mkubwa juu ya shambulizi hilo jipya dhidi ya walinzi wa amani, na amesisitiza kwamba mashambulizi dhidi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa yanaweza kuwa uhalifu wa kivita chini ya sheria za kimataifa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



