Uchumi wa China watarajiwa kufikia lengo la ukuaji wa mwaka huku ukidumisha kasi tulivu katika Novemba

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 16, 2025

Fu Linghui (kulia), Msemaji na Mchumi Mkuu wa Idara ya Taifa ya Takwimu ya China (NBS) na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu Jumuishi ya NBS, akihudhuria mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa na Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China (SCIO) kuhusu hali ya uchumi wa China katika Novemba 2025, mjini Beijing, mji mkuu wa China, Desemba 15, 2025. (Xinhua/Chen Yehua)

BEIJING - Uchumi wa China ulidumisha kasi tulivu katika kipindi cha mwezi Novemba, ukiweka mazingira mazuri ya kufikia lengo la ukuaji la mwaka huu, kama ilivyoonyeshwa na viashiria vya hivi karibuni vya uchumi vilivyotolewa jana Jumatatu na Idara ya Taifa ya Takwimu ya China (NBS).

NBS imesema kwamba viashiria muhimu vya uchumi -- uzalishaji wa viwandani, mauzo ya rejareja na huduma -- viliongezeka mwezi uliopita, wakati huohuo soko la ajira lilidumisha mwelekeo wake tulivu.

"Ikikabiliwa na hali ngumu kutokana na mazingira ya nje yanayobadilika pamoja na hatari na changamoto za ndani, uchumi wa China umedumisha maendeleo tulivu kutokana na uhimilivu wake imara, sera za jumla zinazounga mkono na upanuzi wa vichocheo vipya vya ukuaji," Msemaji wa NBS Fu Linghui ameuambia mkutano na waandishi wa habari.

Kwa mujibu wa takwimu hizo, katika mwezi Novemba, uzalishaji wa viwandani wenye thamani iliyoongezwa wa China uliongezeka kwa asilimia 4.8 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana na katika miezi 11 ya kwanza ya mwaka huu, pato hilo liliongezeka kwa asilimia 6.

Takwimu hizo pia zinaonesha kwamba, mauzo ya rejareja ya bidhaa za matumizi, kiashiria muhimu cha nguvu ya matumizi, yaliongezeka kwa asilimia 4 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana katika miezi 11 ya kwanza, yakifikia jumla ya yuan trilioni 45.61 (dola za Marekani karibu trilioni 6.45), wakati huohuo katika mwezi Novemba pekee, mauzo ya rejareja ya bidhaa za matumizi yaliongezeka kwa asilimia 1.3.

Kwa mujibu wa takwimu hizo, sekta ya huduma pia ilirekodi upanuzi thabiti mwezi uliopita, huku kiwango cha uzalishaji wa huduma kikipanda kwa asilimia 4.2 kikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.

Katika upande wa ajira, takwimu hizo zinaonyesha kwamba soko la ajira la China limeendelea kuwa tulivu kwa ujumla, huku kiwango cha ukosefu wa ajira mijini kilichofanyiwa utafiti kikiwa asilimia 5.1 mwezi Novemba ambapo kwa miezi 11 ya kwanza, kiwango hicho kilikuwa katika asilimia 5.2 kwa wastani.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, Fu amesisitiza ukuaji dhahiri wa nguvu mpya za uzalishaji zenye sifa bora, ambazo zimeingiza nguvu mpya katika maendeleo ya uchumi.

Msemaji huyo pia amesema kuwa mashirika ya kimataifa hivi karibuni yameongeza makadirio yao kuhusu ukuaji wa China, ikionyesha imani ya jumuiya ya kimataifa kwa uchumi wa China.

Fu Linghui (kulia), Msemaji na Mchumi Mkuu wa Idara ya Taifa ya Takwimu ya China (NBS) na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu Jumuishi ya NBS, akihudhuria mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa na Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China (SCIO) kuhusu hali ya uchumi wa China katika Novemba 2025, mjini Beijing, mji mkuu wa China, Desemba 15, 2025. (Xinhua/Chen Yehua)

Fu Linghui (kulia), Msemaji na Mchumi Mkuu wa Idara ya Taifa ya Takwimu ya China (NBS) na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu Jumuishi ya NBS, akihudhuria mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa na Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China (SCIO) kuhusu hali ya uchumi wa China katika Novemba 2025, mjini Beijing, mji mkuu wa China, Desemba 15, 2025. (Xinhua/Chen Yehua)

Picha iliyopigwa Desemba 14, 2025 ikionyesha kituo cha uzalishaji cha kampuni ya viwanda vizito vya usafirishaji wa habarini kwenye eneo la maendeleo ya viwanda vya teknolojia ya hali ya juu la Jiangdu katika Mkoa wa Jiangsu, mashariki mwa China. (Picha na Ren Fei/Xinhua)

Wafanyakazi wakionekana kwenye karakana ya kampuni ya viwanda vizito vya usafirishaji wa baharini kwenye eneo la maendeleo ya viwanda vya teknolojia ya hali ya juu la Jiangdu katika Mkoa wa Jiangsu, mashariki mwa China, Desemba 15, 2025. (Picha na Ren Fei/Xinhua)

Wafanyakazi wakiunganisha sehemu za mashine ya kuchimba handaki kwenye kituo cha uzalishaji cha Kundi la Kampuni za Sayansi na Viwanda la Shirika la Reli la China mjini Wuhan, Mkoani Hubei, katikati mwa China, Desemba 15, 2025. (Picha na Zhao Juni/Xinhua)

Mfanyakazi akitengeneza kalibu kwenye karakana ya kampuni ya kalibu katika Tarafa ya Xingren katika mji wa Nantong, Mkoa wa Jiangsu, mashariki mwa China, Desemba 15, 2025. (Picha na Zhai Huiyong/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha