Rais Zelensky aona mazungumzo ya Berlin yamepata maendeleo huku Ujerumani ikitangaza nafasi ya amani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 16, 2025

Jengo la Reichstag likionekana mjini Berlin, Ujerumani, Desemba 15, 2025. (Xinhua/Zhang Haofu)

Jengo la Reichstag likionekana mjini Berlin, Ujerumani, Desemba 15, 2025. (Xinhua/Zhang Haofu)

BERLIN - Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine amehitimisha mazungumzo ya siku mbili jana Jumatatu na wawakilishi wa Marekani mjini Berlin, Ujerumani akiyaelezea kuwa "yenye matunda," huku Chansela wa Ujerumani Friedrich Merz akisema maendeleo mapya ya kidiplomasia hivi karibuni imeufanya usimamishaji vita nchini Ukraine uwe wenye kuwezekana.

Majadiliano kati ya Zelensky na mjumbe maalum wa Rais Donald Trump wa Marekani Steve Witkoff na mkwewe Trump Jared Kushner yaliendelea kwa saa kadhaa siku za Jumapili na Jumatatu.

Akizungumza baadaye jana Jumatatu kwenye Mkutano wa 8 wa Baraza la Biashara kati ya Ujerumani na Ukraine mjini Berlin, Rais Zelensky amesema mazungumzo muhimu na upande wa Marekani huwa tata na magumu kila wakati, lakini mara hii imepata matunda makubwa. Amesisitiza hitaji la kulinda heshima ya Ukraine na akasema juhudi za kidiplomasia za kumaliza mgogoro huo zitaendelea.

Mpatanishi mkuu wa amani wa Ukraine, Rustem Umerov, ameandika kupitia jukwaa la mtandao wa kijamii X kwamba mazungumzo hayo yamekuwa ya kiujenzi, huku "maendeleo halisi yakipatikana."

Umerov ameongeza kuwa timu ya Marekani inayoongozwa na Witkoff na Kushner "inafanya kazi kwa njia ya kiujenzi sana" kusaidia Ukraine kupata njia ya kufikia makubaliano ya amani ya kudumu.

Gazeti la Ujerumani Die Welt liliripoti kwamba wapatanishi wa Marekani walikuwa wakiishinikiza Ukraine kuachilia eneo la Donbas kama sehemu ya makubaliano hayo.

Alipoulizwa kwenye mkutano na waandishi wa habari jana Jumatatu kama Marekani ilikuwa ikiitaka Ukraine ijiondoe kutoka kwenye ardhi inayoidhibiti, Rais Zelensky amesema Marekani haikutoa madai yake kuhusu ardhi. Hata hivyo, amekiri kwamba Ukraine na Marekani bado zina misimamo tofauti kuhusu masuala hayo.

Kwenye mkutano huo huo na waandishi wa habari, Chansela Merz amesema kwamba Marekani imetoa uhakikisho wa usalama, na kwamba maendeleo mapya ya kidiplomasia imeufanya usimamishaji vita nchini Ukraine uwe wenye kuwezekana.

Kundi la viongozi wa Ulaya, wakiwemo Chansela Merz, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni, Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer, na Rais wa Kamisheni ya Ulaya Ursula von der Leyen, jana Jumatatu jioni walitoa taarifa ya pamoja wakikaribisha "maendeleo hayo makubwa."

Viongozi hao wameahidi kufanya juhudi kwa pamoja ili kutoa uhakikisho imara wa usalama, ikiwemo kudumisha vikosi vya Jeshi la Ukraine katika kiwango cha wakati wa amani cha wanajeshi 800,000.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha