Huawei yafanya semina juu ya elimu ya teknolojia za kisasa na huduma za matibabu kwa mawasiliano kutoka mbali nchini Tunisia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 16, 2025

Watu wakihudhuria semina mjini Tunis, Tunisia, Desemba 15, 2025. (Picha na Adel Ezzine/Xinhua)

Watu wakihudhuria semina mjini Tunis, Tunisia, Desemba 15, 2025. (Picha na Adel Ezzine/Xinhua)

TUNIS - Kampuni kubwa ya teknolojia ya China, Huawei na Kituo cha Mambo ya Kompyuta cha Al-Khawarizmi cha Tunisia (CCK) kwa pamoja zilifanya semina jana Jumatatu mjini Tunis, kwa lengo la kuboresha elimu ya teknolojia za kisasa na huduma za matibabu kwa mawasiliano kutoka mbali nchini Tunisia.

Waziri wa Elimu ya Juu na Utafiti wa Sayansi wa Tunisia Mondher Belaid amesema kwenye semina hiyo kwamba dunia inapitia mapinduzi ya kiteknolojia ambayo hayajawahi kutokea, ikiwa ni pamoja na maendeleo ya haraka ya AI, data kubwa, majukwaa mbalimbali ya kisasa ya kidijitali, usalama wa mtandao wa intaneti, na miundombinu ya kizazi cha siku za baadaye, akisema kuwa Tunisia itatumia teknolojia hizo mpya kujenga mustakabali bora na salama.

Belaid amesema Tunisia inatarajia kuimarisha ushirikiano na washirika katika nyanja zinazoibuka za teknolojia ili kuboresha ubora wa elimu ya juu na utafiti wa kisayansi, usalama wa chakula, kubadilisha muundo wa nishati, huduma za afya, usimamizi wa kiumma wa kidijitali, na nguvu ya ushindani wa kiuchumi.

Mkurugenzi Mkuu wa CCK, Saoussen Krichen, amesema kwamba ushirikiano na Huawei umekuwa na matokeo makubwa katika mazingira ya kiteknolojia ya Tunisia.

CCK hutoa huduma za intaneti kwa sekta ya elimu ya juu na utafiti wa kisayansi nchini Tunisia.

Feng Qiyou, Mkuu wa Huawei Cloud Kaskazini mwa Afrika, amesema kwamba Huawei na CCK zimezindua kwa pamoja jukwaa la kwanza kwa ajili ya huduma za wingu za utafiti wa elimu na sayansi katika eneo la Kaskazini mwa Afrika, ambalo linafikia taasisi zaidi ya 450 za elimu na utafiti na kutoa huduma kwa vyuo vikuu 14 nchini Tunisia, likichangia "uungaji mkono wa pande zote" kwa ajili ya ushirikiano wa kisayansi, mafunzo ya mtandaoni, na kunufaika pamoja na rasilimali.

Feng ameongeza kuwa programu za AI kwenye jukwaa hilo zimetekeleza kwa mafanikio upigaji wa picha za kimatibabu unaoendeshwa na AI, ambayo imeongeza kwa kiasi kikubwa ufanisi wa huduma za matibabu kwa mawasiliano kutoka mbali nchini Tunsia.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha