Marekani yapanua orodha ya nchi zinazowekewa vizuizi kuingia Marekani

(CRI Online) Desemba 17, 2025

Rais Donald Trump wa Marekani jana Jumanne alisaini tamko linalopanua orodha ya nchi zinazowekewa vizuizi kamili au kwa sehemu vya kuingia nchini humo.

Ikulu ya Marekani imesema kwenye taarifa yake ya uhalisi wa hali kuwa Rais Trump amesaini amri hiyo ikipanua na kuimarisha vizuizi kwa raia kutoka nchi zinazojulikana kuwa na upungufu mkubwa, sugu, na mbaya katika ukaguzi wa watu, uhakiki, na kubadilishana taarifa ili kulinda taifa kutoka kwenye usalama wa taifa na matishio ya usalama wa umma.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, amri iliyosainiwa na Rais Trump imeongeza vizuizi kamili na vikwazo vya kuingia kwa nchi za ziada tano ambazo ni Burkina Faso, Mali, Niger, Sudan Kusini, na Syria. Pia inaongeza vizuizi hivyo kwa watu wenye pasi za kusafiria zilizotolewa na Mamlaka ya Palestina.

Amri hiyo pia imeweka vizuizi kwa sehemu kwa nchi nyingine 15, ikiwa ni pamoja na Angola, Malawi, Tanzania, Zambia na Zimbabwe.

(Wahariri wa tovuti:Zhao Jian)

Picha