Rais Xi Jinping asikiliza ripoti ya kazi aliyotoa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Hong Kong

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 17, 2025

Rais Xi Jinping akikutana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong (HKSAR) John Lee, ambaye amekuja Beijing kutoa ripoti ya kazi. Desemba 16, 2025. (Xinhua/Yin Bogu)

Rais Xi Jinping akikutana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong (HKSAR) John Lee, ambaye amekuja Beijing kutoa ripoti ya kazi, Desemba 16, 2025. (Xinhua/Yin Bogu)

BEIJING - Rais Xi Jinping jana Jumanne alikutana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong (HKSAR) John Lee, ambaye yuko katika ziara ya kikazi mjini Beijing. Rais Xi alisikiliza ripoti ya kazi aliyotoa Lee kuhusu hali ya sasa ya Hong Kong na kazi ya serikali ya HKSAR.

Rais Xi amesema kwamba serikali kuu ya China inatambua vya kutosha kazi ya Lee na serikali ya HKSAR.

"Mkutano wa nne wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China ulisisitiza umuhimu wa kutekeleza kithabiti sera ya 'nchi moja, mifumo miwili', ambayo chini yake watu wa Hong Kong wanajitawala Hong Kong kwenye kiwango cha juu, na kuhimiza ustawi na utulivu wa muda mrefu wa Hong Kong," Rais Xi ameeleza.

Ametoa wito kwa serikali ya HKSAR kuufanya utendaji kazi wake katika kufungamana na Mpango wa 15 wa Maendeleo ya Miaka Mitano, kushikilia na kukamilisha uongozi wa mambo ya utawala ya serikali yake, kuhimiza kwa hatua madhubuti maendeleo ya uchumi yenye sifa bora, na kushiriki kwa kina kwenye maendeleo ya Eneo la Ghuba Kuu ya Guangdong-Hong Kong-Macao, ili Hong Kong kufanya mafungamano mazuri kati yake na mambo makuu ya maendeleo ya kitaifa.

Rais Xi Jinping akikutana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong (HKSAR) John Lee, ambaye yuko katika ziara ya kikazi mjini Beijing, Desemba 16, 2025. (Xinhua/Yin Bogu)

Rais Xi Jinping akikutana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong (HKSAR) John Lee, ambaye yuko katika ziara ya kikazi mjini Beijing, Desemba 16, 2025. (Xinhua/Yin Bogu)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha