Ripoti yaonesha mustakabali wa sekta ya magari upo katika ushirikiano na China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 17, 2025

Wafanyakazi wakiunganisha sehemu za gari kwenye mstari wa uzalishaji wa Kiwanda cha Kampuni ya Magari ya Kibiashara yenye Kutumia Nishati Mpya ya Weichai katika Eneo la Wendeng la Mji wa Weihai, Mkoa wa Shandong, Mashariki mwa China, Julai 21, 2023. (Xinhua/Guo Xulei)

FRANKFURT - Ripoti iliyotolewa na Kituo cha Utafiti wa Magari (CAR) cha Ujerumani Jumatatu wiki hii imesema kuwa soko la magari ya abiria duniani linatarajiwa kufikia rekodi mpya ya juu mwaka 2025, na mustakabali wake utategemea zaidi ushirikiano na China.

Kwa mujibu wa makadirio ya Kituo hicho, mauzo ya magari ya abiria duniani yanatarajiwa kufikia magari milioni 81.3 mwaka huu wa 2025, ambacho ni kiwango cha juu zaidi katika miaka minane iliyopita na kwamba China inaendelea kubeba jukumu muhimu katika uzalishaji na mahitaji.

Mkurugenzi wa CAR Ferdinand Dudenhoeffer amesema kuwa soko kubwa na mnyororo jumuishi wa usambazaji wa China vinatoa faida za uchumi wa kiwango zinazoongezeka, wakati huohuo maendeleo katika betri za umeme, magari yanayotumia nishati mpya, na teknolojia ya magari yanayojiendesha yenyewe yakibadilisha sekta ya magari duniani.

"Yeyote ambaye hayupo China hayupo kwenye biashara ya magari," amenukuliwa akisema kwenye ripoti hiyo.

Miongoni mwa masoko 15 makubwa zaidi ya magari duniani, mauzo ya magari ya abiria nchini China, Marekani, India, na Uturuki yanatarajiwa kuongezeka kwa zaidi ya asilimia 4 mwaka 2025.

Kwa upande mwingine, masoko makubwa ya Ulaya yanatarajiwa kuwa chini ya matarajio, huku mauzo nchini Ujerumani yakiongezeka kwa asilimia 0.7 pekee, wakati Ufaransa na Italia yakikadiriwa kushuhudia upungufu wa asilimia 4.8 na 2.6, mtawalia.

Picha hii iliyopigwa Novemba 3, 2025 ikionyesha mstari wa kuunganisha magari yanayotumia nishati mpya (NEV) wa BYD, mtengenezaji mkuu wa magari ya NEV nchini China, kwenye kiwanda cha BYD mjini Zhengzhou, Mkoani Henan, katikati mwa China. (Xinhua/Li Jianan)

Kwa mtazamo wa mwaka 2026, CAR inatarajia mauzo duniani kuongezeka kwa asilimia 2.6 hadi kufikia magari milioni 83.4 duniani kote. Asia inakadiriwa kupita ukuaji huo, kwa ongezeko la asilimia 3.8, linalotokana hasa na sehemu inayoongezeka ya uzalishaji na mauzo ya China.

Mwaka 2025, zaidi ya asilimia 60 ya uzalishaji wa magari ya abiria duniani umetokea Asia, ikilinganishwa na takriban asilimia 15 barani Ulaya, kwa mujibu wa ripoti hiyo. Inaonesha kuwa Ujerumani na wazalishaji wengine wa Ulaya wanatarajiwa kupoteza sehemu yao zaidi mwaka 2026, kwani wamekabiliwa na ongezeko la ushindani duniani na athari za sera za ushuru za Marekani.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha