Lugha Nyingine
Kampuni za China na Kenya zasaini mkataba wenye thamani ya Dola milioni 250 kuongeza uzalishaji wa saruji
Kampuni ya Saruji ya Kenya Bamburi imesaini mkataba wa uhandisi, manunuzi na ujenzi wenye thamani ya Dola milioni 250 za Kimarekani na kampuni ya ujenzi ya CBMI ya China kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda kipya cha kusaga mawe ya simenti (clinker) kwenye kaunti ya Kwale.
Akiongea jana Jumanne mjini Nairobi kwenye hafla ya kusaini makubaliano, Rais William Ruto amesema mstari mpya wa uzalishaji wa clinker ni aina ya uwekezaji unaoleta mabadiliko yanayohitajika kwenye uwekezaji unaoleta mageuzi yanayochochea maendeleo ya Kenya, kupitia uungaji mkono wa makusudi kwenye uwekezaji wa umma na binafsi.
Rais Ruto ameuelezea mradi huo kuwa utatoa mchango muhimu katika kuimarisha uwezo wa kiviwanda wa Kenya, na kuunga mkono ujenzi wa miundombinu ya kimkakati ya taifa, pamoja na programu ya makazi ya nafuu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



