Lugha Nyingine
China yazindua uendeshaji maalum wa forodha kisiwani kote kwenye Bandari ya Biashara Huria ya Hainan (5)
![]() |
| Lori lililobeba shehena ya kwanza ya bidhaa zilizopitia utaratibu wa forodha likionekana kwenye eneo la ukaguzi katika Bandari ya Xinhai na Bandari ya Nangang, ambazo ni bandari mbili za forodha za "mstari wa pili", huko Haikou, Mkoa wa Hainan, kusini mwa China, Desemba 18, 2025. (Xinhua/Pu Xiaoxu) |
HAIKOU - China jana Alhamisi imezindua rasmi uendeshaji maalum wa forodha kisiwani kote katika Bandari ya Biashara Huria ya Hainan (FTP), ambayo ni bandari ya bishara huria kubwa zaidi duniani kwa ukubwa wa eneo lake, ikiruhusu kuingia kwa uhuria zaidi kwa bidhaa za nje, na kupanua wigo wa kusamehe ushuru kwa bidhaa na kutoa hatua zaidi za kusaidia biashara.
Hatua hiyo imechukuliwa zaidi kuwa ni hatua alama ya China kuendelea kuhimiza biashara huria na kupanua ufunguaji mlango kwa vigezo vya juu katika wakati huu wa kutokea zaidi kwa vitendo vya kujilinda kibishara duniani kote.
Kutokana na mpango huo mpya, kisiwa hicho cha kitropiki chenye ukubwa wa kilomita za mraba zaidi ya 30,000 kimeteuliwa kuwa eneo maalum la usimamizi na udhibiti wa forodha.
Hii ni alama ya kipindi kipya katika maendeleo ya Bandari ya Biashara Huria ya Hainan, ambapo mzunguko wa bidhaa, mitaji, watu na data za takwimu utakuwa huria zaidi, na unaoungwa mkono kwa kupitia hatua za kusaheme ushuru, kodi za chini na utaratibu wa kodi uliorahisishwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




