Lugha Nyingine
Shughuli za Utalii wa kitamaduni zachochea ustawi wa Kijiji cha Manhai, Mkoa wa Yunnan, China (5)
Kijiji cha Manhai, kilichopo katika Wilaya Inayojiendesha ya Kabila la Wahani ya Mojiang ya Mji wa Pu'er katika Mkoa wa Yunnan, kusini magharibi mwa China, ni maskani kwa watu wa makabila mbalimbali. Katika miaka ya hivi karibuni, kwa msaada wa serikali ya mtaa, kijiji hicho kimepata maendeleo ya dhahiri katika ustawi wa kijiji.
Kijiji hicho cha Manhai kimebadilisha nyumba zisizotumika kuwa nyumba za kupokea wageni na vituo vya ziara za masomo. Kijiji hicho pia kimetumia mali ya urithi wake wa utamaduni usioshikika, kama vile kusuka mianzi kwa kuanzisha madarasa ya ziara za masomo na bidhaa za ubunifu wa kitamaduni. Aidha, kijiji hicho cha Manhai kimewapa mafunzo wanakijiji ya namna ya kuendesha nyumba za kuwapokea wageni na kuwa waelekezaji wakati wa ziara za masomo. Hivi sasa kijiji hicho kimevutia watalii na wajasiriamali wengi kutembelea na kuanzisha biashara huko.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




